Recent Posted

Kijana Mbunifu wa Vipindi - Global TV ONLINE

-


Global TV ONLINE ni televisheni ya kwenye mtandao inayafuatiliwa na watu wengi duniani,
inahitaji kijana mwenye uwezo na ari ya kuipeleka mbele TV hiyo mwenye sifa zifuatazo: -Anahitajika kijana wa kiume Mbunifu, Mwenye Ari kubwa va kazi ya Social Media, Mfuatiliaji wa matukio ya kitaifa na kimataifa kihabari na anayeweza kujituma., kuongoza wenzake na kufanya kazi bila ya kusimamiwa na kuleta tija Global Tv.

Kijana Mwenye Sifa Hizo anatakiwa awe na  uwezo na ujuzi wa kutosha wa kubuni, kuandaa na kuendesha vipindi vya televisheni.. Aidha, anatakiwa awe na uwezo na ujuzi wa kupiga na kuhariri  picha za video kwa ubora wa hali ya juu. (CAMERAMAN CUM VIDEO EDITOR)

Mwisho: Kama unafikiri unazo sifa Zilizotajwa hapo, niandikie barua ya kujieleza ikiambatana na vielelezo vyako. Kujieleza kwanini unadhani unastahili kupewa kazi hiyo ni muhimu kuliko kuambatanisha CV yako. Maelezo yako elekeza kwa:-

MENEJA MKUU
S.L.P 7534
DAR ES SALAAM

Wasilisha mwenyewe ofisini kwetu, Sinza Bamaga (Nyuma ya TSN Petrol Station). Simu: 022 2773356 au 0715 a 288627. Mwisho wa ku okea maombi ni Septemba 2016



No comments